TAARIFA YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI DHIDI YA MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO - CHADEMA
Mimi
FABIAN L. SKAUKI, Mgombea Ubunge wa Uchaguzi mdogo Jimbo la CHALINZE
kwa tiketi ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi mgombea
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba amepoteza sifa
za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo:
1.
Ndugu MATHAYO M. TORONGEY amejaza taarifa za uongo kwenye fomu yake
kwamba kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka
vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.
2.
Ndugu MATHAYO M. TORONGEY amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma
na kuandika Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea
huyu hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba
amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea.
0 comments:
Post a Comment