Home » » WANANCHI RUKWA WAUNGAMKONO SERIKALI KUTENGA BAJETI MAALUM KUKABILIANA NA VIFO VYA UZAZI

WANANCHI RUKWA WAUNGAMKONO SERIKALI KUTENGA BAJETI MAALUM KUKABILIANA NA VIFO VYA UZAZI

Written By kitulofm on Monday, 17 March 2014 | Monday, March 17, 2014


Daktari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, John William Gurisha akitoa takwimu za afya ya Uzazi Mkoani Rukwa katika maadhimisho hayo.
Daktari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, John William Gurisha akitoa takwimu za afya ya Uzazi Mkoani Rukwa katika maadhimisho hayo.
IMG_4189

Washiriki anuai kutoka Mkoa wa Rukwa wakiwa katika picha za matukio.
Baadhi ya washiriki wa sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya Utepe Mweupe.
Baadhi ya washiriki wa sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya Utepe Mweupe.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Evidence for Action Tanzania, Craig John Ferla, kupitia kampeni ya Mama Ye akichangia damu.Zaidi ya chupa 970 za damu zilipatikana katika maadhimisho ya wiki ya utepe mweupe.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Evidence for Action Tanzania, Craig John Ferla, kupitia kampeni ya Mama Ye akichangia damu.Zaidi ya chupa 970 za damu zilipatikana katika maadhimisho ya wiki ya utepe mweupe.

ZAIDI ya wananchi 16,828 wa Mkoa wa Rukwa wamesaini ombi la haki (petition), wakiiomba Serikali kutenga bajeti mahususi ili kuviinua vituo vya afya nchini viweze kutoa huduma za dharura kwa za uzazi ikiwemo upasuaji, damu salama, vifaa vya kutosha na wafanyakazi wenye ujuzi.
Taarifa hiyo imetolewa na Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay jana mjini hapa mbele ya mgeni rasmi wa siku ya Utepe Mweupe ambaye ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.
“Lengo ni kuhakikisha bajeti ya kutosha inatengwa na Serikali Kuu pamoja halmashauri ili kuhakikisha kuwa angalau asilimia 50 ya vituo vya afya nchini vinatoa huduma za dharura za uzazi,” alisema Mlay.
Kwa Upande wake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika ujumbe wake ameziagiza mara moja halmashauri zote nchini kutenga bajeti ya kutosha ili kuimarisha vituo vya afya viweze kutoa huduma za dharura za uzazi ikiwamo upasuaji lengo likiwa ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Tamko hilo lipo katika hotuba ya Waziri Pinda iliyosomwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akimwakilisha Waziri Mkuu. Katika maelezo yake Waziri Pinda alisema vifo vya mama na mtoto baado ni changamoto nchini hivyo Serikali ina kila sababu ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Aliongeza kuwepo kwa huduma hizo na watalaamu kwenye vituo vya afya na hospitali nchini, ni njia pekee itakayosaidia kupunguza vifo hivyo.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm