Mkuu wa shule ya Sekondari Lupalilo Mwl.Liombo amekanusha Taarifa
zilizozagaa kuhusiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Lupalilo kupiga picha
za utupu
Mkuu huyo amesema taarifa hizo si za kweli bali wanafunzi hao wamepiga
picha ambazo haziendani na maadili ya shule za sekondari wilayani Makete na hapa nchini
Akizungumza na kitulo fm mapema hii leo katika kipindi cha Morning Power mara baada ya kupigiwa simu kutoa maelezo ya kina kuhusu taarifa zilizozagaa mitaani kuhusu wanafunzi wa shule ya Lupalilo iliyopo katika kata ya Tandala amesema kuwa taarifa hizo si sahii ukweli ni kwamba wamepiga picha ambazo ni tofauti na maadili mapoja na sheria za shule hiyo
Pia amesema kuwa hatua zilizochukuliwa dhidi yao ni pamoja na kuwaita wazazi wao na kufanya mkutano wa pamoja wazazi na watoto shule nzima kwani wanafunzi waliofanya kosa hilo ni wengi,baada ya hapo walipewa adhabu ya kuchapwa viboko na wazazi wao mbele ya wanafunzi wote wakiwepo wazazi na kupewa adhabu ya kukata kuni na kukwetua barabara mita kadhaa
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment