Chama cha Alliance For Change and Transparency Mkoa wa
Kigoma,kimeshusha Bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
tawi la Ujiji stendi ya zamani na kupandisha bendera ya (ACT) wakati wa
uzinduzi rasmi wa matawi sita katika manispaa ya kigoma ujiji.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Katibu wa ACT Mkoa Athuman Kabogo alidai lengo la kushusha bendera hiyo ni hatua ya kukataa kugeuzwa kuwa vibaraka wa watu wengine kwa kukosa haki ya kuhoji na kuwania nyadhifa za chama hicho na hivyo kuanzisha ACT kama chama cha wanyonge kinachoweza kuwasikiliza na kutoa haki kwa kila mmoja.
0 comments:
Post a Comment