Serikali
wilayani Makete kupitia mhandisi msaidizi wa Idara ya maji imeagiza kampuni ya
ZUBERI inayoshughulikia mradi wa utandazaji wa mabomba katika kijiji cha Ujuni
kata ya kitulo kukamilisha mradi huo mara moja
Agizo hilo
limetolewa Mhandisi msaidizi idara ya maji wilaya ya Makete Bw.Martin Luvanda
mapema hii leo katika kijiji cha Ujuni kata ya Kitulo wilayani Makete Mkoani
Njombe alipotembelea katika kijiji hicho ili kukagua hatua iliyofikiwa na
mkandarasi anayetekeleza kutoka katika
kampuni ya ZUBER Bw.Thomas Maduhu
Naye Afisa mtendaji wa kata hiyo Bw.Christopha Fungo
ameuomba uongozi wa serikali kutoka halmashauri ya wilaya kuusimamia mradi huo
kwa ukaribu zaidi ili mradi huo uweze kukamilika mapema
Mradi huo unaotegemewa kugharimu zaidi ya sh.milioni
mia 2 huku ikiwa imeshatumika zaidi ya milioni 70
0 comments:
Post a Comment