Home » » GAZETI LA DARAJA LAPITISHA MSASA KWA MARIPOTA WA GAZETI HILO VIJIJINI WILAYANI MAKETE

GAZETI LA DARAJA LAPITISHA MSASA KWA MARIPOTA WA GAZETI HILO VIJIJINI WILAYANI MAKETE

Written By kitulofm on Thursday, 6 March 2014 | Thursday, March 06, 2014

Maripota wa gazeti la daraja Letu wilayani Makete mkoani Njombe wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuandika na kuripoti habari kutoka kwenye maeneo yao hii leo katika ukumbi wa Spiritual Centre Makete.
 Mhariri wa gazeti la daraja Letu Robert Zephania (kulia) akimsikiliza mmoja wa maripota akichangia mada katika mafunzo hayo.
Maripota wakimsikiliza kwa umakini Mhariri wa gazeti la daraja letu Robert Zephania 
 Edwin Moshi Mmiliki wa mtandao wa EDDY BLOG,akifafanua jambo kwa maripota wa gazeti la Daraja letu.

Picha na Edwin Moshi

Habari na Furahisha Nundu

Zaidi ya maripota 22 kutoka katika baadhi ya kata zilizopo wilayani Makete wamepata mafunzo ya siku moja jinsi ya kuandika habari za maeneo wanayoishi kutoka Gazeti la Daraja lililopo Mkoani Njombe

Akizungumza katika mafunzo hayo Mhariri wa gazeti la Daraja letu Robert Zefania amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuongeza ufahamu kwa jamii ya wanamakete na watanzania kwa ujumla kwani gazeti hilolimekuwa likitoa changamoto zinazoikabili jamii na wahusika huzifanyia kazi

Akielezea baadhi ya faida zilizopatikana tokea kuanzishwa kwa gazeti hilo amesema kuwa gazeti limekuwa likiibua changamoto nyingi lakini wahusika wamekuwa wakizitendea kazi mara moja ikiwemo wananchi waliokuwa wakilalamikia mbolea aina ya minjingu mara baada ya gazeti hilo kuandika habari hizo serikali imeruhusu mwananchi kuchagua mbolea anayohitaji

Katika mafunzo hayo aliongozana na mwanahabari wa Gazeti hilo Shaban Lupimo ambaye amewaasa maripota hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili waliyopewa,kujiamini,kuandika habari zenye ukweli na uhakika ili kutoleta madhara kwa jamii na msuguano kati yake na chanzo chake cha habari

Maripota hao waliotoka katika kata ya Bulongwa,Matamba,Tandala,Mang’oto,Ukwama ,Lupila ,Ipepo,Ipelele,Iniho,Isapulano,Luwumbu pamoja na Iwawa wamelishukuru gazeti hilo kwani limewajengea uwezo mkubwa wa kujua jambo na kutambua haki za wananchi

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm