Hatimaye
bunge maalum la katiba limemchagua Mh. Samia Suluhu Hassan kuwa makamu
mwenyekiti wa bunge hilo, katika uchaguzi huo uliofanyika muda huu
bungeni Dodoma
Akitangaza
matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo amesema Mh. Samia amepata kura
390 sawa na asilimia 74.6 huku mgombea mwenzake Mh. Amina Abdalah Amour
akipata kura 126, ambapo kura 7 zimeharibika
Kwa matokeo hayo Mh Samia amekuwa makamu mwenyekiti mteule wa bunge maalum la katiba
Akizungumza
mara baada ya kutangazwa, Mh. Samia amesema anamshukuru mpinzani wake
kwa kumpa wakati mgumu ikiwemo kigezo cha kukubalika ndani ya bunge,
pamoja na wanawake wote waliopo ndani ya bunge hilo kwa kumpa ushindi
huo
Awali
Mh. Amina yeye amekubaliana na matokeo hayo, na kuongeza kuwa kwa kuwa
aliyeshinda ni mwanamke, basi ushindi huo ni wa wanawake wote
CHANZO:EDDY BLOG
0 comments:
Post a Comment