Home » » WATATU WAPANDISHWA KIZIMBANI MAKETE AKIWEMO MTOTO MWENYEUMRI WA MIAKA 17

WATATU WAPANDISHWA KIZIMBANI MAKETE AKIWEMO MTOTO MWENYEUMRI WA MIAKA 17

Written By kitulofm on Thursday, 13 March 2014 | Thursday, March 13, 2014

Watu watatu wamepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya mwanzo wilayani Makete kwa makosa tofauti akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Lupila.

Akieleza kutokea kwa tukio hilo mwendesha mashitaka wa polisi PC Ally,mbele ya hakimu Happy Ngogo amesema tukio hilo lilitokea june 26 mwaka jana ambapo mtuhumiwa aliiba mashine yenye thamani ya shilingi milioni moja laki 5 na sabini mali ya Hilali Msawe.

Aidha Ngogo amesema kutokana na sheria inayolinda haki ya mtoto mahakama hiyo ilimkabidhi mtoto huyo chini ya ustawi wa jamii ili kutenda haki ya mtoto huyo.

Hata hivyo washauri wa ustawi wa jamii Bi.Seche na Panga waliamuru mahakama hiyo impe adhabu mtoto huyo.

Hata hivyo mahakama iliamua kumshauri mtoto huyo naye akakubaliana nao na kukiri kosa na kuahidi kurudisha mashine hiyo na mahakama hiyo kumsamehe na kutokumpatia adhabu yoyote.

Katika tukio la pili Julidi Mahenge (21) mkazi wa Ujuni amepandishwa kizimbani leo kwa tuhuma za ubakaji.

Tukio hilo lilitokea March 10 mwaka huu katika kijiji cha Nkenja kata ya Kitulo wilayani hapa mtuhumiwa alifanya tendo la ndoa na mtoto mwenye umri chini ya miaka 18.

Hata hivyo mshitakiwa amekana shitaka linalo mkabili na dhamana iko wazi,amerudishwa mahabusu kwa kukosa wadhamini hadi Marchi 21 mwaka huu kesi itakapo tajwa tena.

Wakati huo huo Tumlack msigwa (21) mkazi wa kitulo amepandishwa kizimbani kwa kosa la unyang`anyi wa kutumia nguvu.

Mwendesha mashitaka wa polisi PC Ally mbele ya hakimu Heppy Ngogo ameeleza kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Marchi 10 mwaka huu ambapo alimkaba na kufanikiwa kumpora  Pelesi Mwaigaga shilingi laki 7

Hata hivyo mshitakiwa amekana shtaka hili na dhamana iko wazi amerudishwa tena mahabusu kwa kukosa wadhamini hadi Marchi 21 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Mwendesha mashitaka Kess Ally ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea March 10 mwaka huu saa nne usiku


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm