Idara
ya maji wilayani Makete mkoani Njombe imejipanga kuhakikisha wakazi wa
Makete mjini watapata maji kwa asilimia mia moja ifikapo Mei mwaka huu
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja wa mamlaka ya maji Makete mjini Bw. Yonasi
Ndomba wakati akizungumza na mtandao huu katika wiki hii ya kuelekea
kilele cha siku ya Maji duniani ambacho kwa mkoa wa Njombe
kitaadhimishwa katika wilaya ya Makete katika viwanja vya mabehewani
Bw.
Ndomba amesema kwa sasa ni asilimia 4 tu ya wakazi wa Makete mjini
hawapati maji saa 24, hivyo kutokana na mikakati wanayeoendelea
kuitekeleza kwa sasa, wanaimani hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu maji
makete mjini yatapatikana kwa asilimia mia moja
Akizungumzia
kilele cha wiki ya maji, amesema kimkoa maadhimisho yatafanyika
wilayani hapa na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe
Kapteni mstaafu Aseri Msangi, ambapo amewataka wananchi kujitokeza kwa
wingi katika maadhimisho hayo
Mkuu
wa mkoa anatarajiwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa tanki la maji
lililopo Mwongolo, Makete mjini pamoja na mkutano wa hadhara
utakaofanyika katika viwanja vya mabehewani pamoja na burudani
mbalimbali kutoka kwenye vikundi vya sanaa vilivyopo wilayani hapo
Kwa
upande wake Kaimu mhandisi wa maji wilaya ya Makete Bw. Nahom Tweve
ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kuchunga mifugo kwenye vyanzo
vya maji kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha maji kuzidi kupungua
wilayani hapo, hivyo adha ya maji itazidi kuongezeka badala ya kupungua
Amesema
kwa kuwa sheria zipo, yeyote atakayekamatwa na serikali akiharibu
vyanzo vya maji atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho
kwa wengine wenye tabia kama hiyo
"Miaka
30 iliyopita ndani ya wilaya hii kuna mito ilikuwa huwezi kuvuka
kutokana na wingi wa maji, wapo wazee waliokuwepo enzi hizo watakuwa ni
mashaidi, lakini kwa sasa mito hiyo unajivukia biala wasiwasi kwa kuwa
maji yamepungua sana" amesema Tweve
Kaimu
huyo amesema ni lazima kila mmoja wetu atunze vyanzo vya maji kwa
manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo, kwa kuacha kuchunga mifugo
kwenye vyanzo vya maji, kupanda miti ambayo ni rafiki na vyanzo vya maji
pamoja na kuacha uharibifu wowote ule kuhusu vyanzo vya maji
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "uhakika wa maji na nishati"
0 comments:
Post a Comment