
Na Yonna Mgaya IRINGA
Mazingira
hatarishi na matatizo ya kisaikolojia ni miongoni mwa mambo yanayopelekea
vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi amesema baadhi ya watu
wamepelekea kufanyiwa vitendo vya unyanyasi wa kijinsia kwa kuweka mazingira
hatarishi.
Amesema
ili kuepusha vitendo vya ukatili ni vyema jamii ikatambua elimu ya ulinzi na
salama kwa kutembea kwa makundi nyakati za usiku kwa lengo la kupambana na
vitendo hivyo.
Kamanda
Mungi amesema uwepo wa vitendo vya kujitoa maisha ikiwemo kujinyonga mkoani
Iringa kumetokana watu kuwa na maisha duni, kukosa matumaini ya kupona na
msongo wa mawazo.
Hata hivyo, Kamanda wa jeshi la polisi amesema jeshi lake linaendelea
kutoa elimu kwa jamii kuhusu elimu ya kujitambua kwa lengo la kupunguza matukio
ya uharifu ndani ya jamii.
0 comments:
Post a Comment