Wafanya
biashara wilayani makete wameshauriwa kufanya biashara eneo moja ambalo
litakuwa lipendekezwa na serikali ya kijiji au halmashauri kwa biashara ya
vinywaji na biashara za maduka ya rejareja ili kurahisiaha mzunguko wa biashara
,ulizi wa usalama na utoaji wa huduma kwa jamii
Picha na Maktaba,Habari na Henrick Idawa
Hayo
yamezungumzwa na afisa biashara wilaya ya makete bw,edonia mahenge katika kikao
na wafanyabishara wa kijiji cha lupila kata ya lupila akiwasihi wafanya
biashara hao kuhamia eneo la itundu ambalo kwa sasa linatumika kwama soko kila
siku ya alhamisi jumapili na mnada katika eneo hilo .
Pia
bw. Mahenge ameelezea namna na umhimu wa kulipia leseni ya biashara ambapo
amesema serikali ili kuondoa usumbufu inaweka form za upataji wa leseni kwa
watendaji wa vijiji ili kurahisisha
taratibu za leseni kwa wafanya biashara katika eneo husika.
Nao
wafanya biashara walipopewa nafasi ya kuuliza maswali wamelalamikia ubovu wa
miundo mbinu ya barabara za kuingia katani hapo,bidhaa ziletwazo kupitia minada
kuisha muda wa matumizi licha ya kuridhia kuhamia eneo hilo
la soko la itundu kufanyia biashara na wameazimia kufikia tarehe 6.april mwaka
huu kila mfanya biashara anatakiwa kufanyia biashara eneo hilo .
0 comments:
Post a Comment