Mtoto Njiti akiwa amebebwa na mama yake.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
WANAWAKE
Mkoani Singida wamehimizwa kujenga tabia ya kuwakumbuka wanawake wenzao
waliofungwa na walioko mahabusu gerezani ili waendelee kuaminiwa kuwa
bado ni sehemu muhimu ya wanawake mkoani humu.
Wito
huo umetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake kanisa
la Free Pentekoste church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida mjini,
Lessi Jaredi muda mfupi baada ya kutoa msaada wa vitu mbali mbali kwa
wanawake wanatumikia adhabu jela na wale walioko mahabusu katika gereza
la wilaya ya Singida.Msaada huo ulikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku
ya wananwake duniani.
Amesema
wanawake waliopo magerezani, hawajapoteza utu wao na wala sio kwamba
hawana msaada tena katika kuchangia maendeleo ya mkoa wa Singida na
taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment