Mshindi wa nishani ya Nobel ya fasihi Doris Lessing amefariki. Akiwa ni mzaliwa wa Iran mwaka 1919, lakini wazazi wake wakiwa Waingereza , Lessing alikulia kusini mwa Afrika kabla ya kuhamia Uingereza.
Aliandika kitabu chake cha kwanza nchini Uingereza , kilichojulikana kama " The Grass Is Singing", Majani yanaimba.
Aliwahi kusema kuwa anafurahia kuandika kuhusu kitu chochote.
Ameongeza kuwa hakuna furaha kama wakati una hadithi nzuri kichwani mwako na kuanza kuiandika.
Amefariki akiwa na umri wa miaka 94.
0 comments:
Post a Comment