![]() |
| Mhudumu wa Hospitali ya Muhimbili akimrejesha Joseph Yona wodini baada ya kufanyiwa matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha MOI, Dar es Salaam jana. |
Mgogoro unaoendelea ndani ya Chadema una uhusiano na tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa Wilaya ya Temeke, Joseph Yona, Polisi imesema.
Hatua za awali za upelelezi wa tukio hilo kwa mujibu wa Polisi, kimazingira zinaonesha kuwa linatokana na mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho, huku kukiwa hakuna chanzo kingine kinachohusishwa.

0 comments:
Post a Comment