Home » » CHAMA CHA WAFANYAKAZI NYANDA ZA JUU KUSINI WATEMBELEA BWAWA LA MTERA

CHAMA CHA WAFANYAKAZI NYANDA ZA JUU KUSINI WATEMBELEA BWAWA LA MTERA

Written By kitulofm on Sunday, 2 February 2014 | Sunday, February 02, 2014

Wafanyakazi wametakiwa kuwa na mshikamano katika sehemu zao za kazi ili kuongeza ufanisi wa kazi maofisini.
 
Hayo yamesemwa na Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa viwanda, biashara, tasisi za fedha, huduma na ushauri (TUICO) Nyanda za juu kusini Bwana Merboth Kapinga walipokwenda kutembelea mgodi wa Mtera.
 
Bwana Kapinga amewaambia wajumbe wa chama cha wafanyakazi kuwa nguvu ya chama ni wafanyakazi wenyewe kushirikiana kwa pamoja na kuzilinda mali za maofisini mwao.

Katibu wa chama cha wafanyakazi(TUICO) Nyanda za Juu Kusini Ndugu Merboth Kapinga akizungumza na wafanyakazi Walipotembelea bwawa la Mtera.

Aidha Bwana Kapinga amewataka wakuu wa idara kuwaelimisha wafanyakazi juu ya umuhimu wa kazi zao pia amewataka wafanyakazi wa ngazi za chini kukaa kikao na kujadili na kutoa mawazo tofauti tofauti kwa wakuu wa idara ili yaweze kupelekwa kwenye ngazi za juu.
 
Hata hivyo wafanyakazi walitembelea bwawa la Mtera walifurahishwa na ziara hiyo iliyowapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii ili kuilinda na kuliendeleza taifa la Tanzania.

Kaimu meneja wa tanesco tawi la Mtera Ndugu Salum Omar Njipwili akitoa shukrani zake kwa wafanyakazi wa Nyanda za Juu kusini.

Wafanyakazi kutoka nyanda za juu kusini na tawi la tanesco Mtera wakisikiliza kwa makini kikao cha viongozi wa TUICO.
Pia wafanyakazi wa tanesco wakishirikiana na  Kaimu Meneja wa Tanesco tawi la Mtera Bwana Salum Omar Njipwili  walifurahishwa na ujio wa wafanyakazi kutoka nyanda za juu kusini hivyo wamewataka kuja kutembelea mara kwa mara ili kujifunza mambo mengi zaidi.


Wafanyakazi wa Nyanda za Juu kusini wakiwa na wafanyakazi wa Tanesco tawi la Mtera katika picha ya pamoja.
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm