Vikao vya Bunge Maalum la Katiba vimendelea tena leo kwa kujadili sura ya 1 na ya ile ya 6 ya Rasimu ya Katiba licha ya baadhi ya wajumbe kususia kikao hicho jana jioni na kutoka nje ya ukumbi kwa kile walichodai ni kuchoshwa na matusi, dharau na ubaguzi .
Kauli
ya kuendelea kwa kikao leo ilitolewa usiku wa jana na Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, Jaji Federick Werema kabla ya kuahirishwa kwa kikao cha
jioni cha Bunge hilo, wakati aliposimama kutoa hoja ya kutengua Kanuni
za Bunge Maalum la Katiba ili kuongeza muda wa kujadili sura hizo, kutoka 3 hadi siku saba.
Kabla
kutengua, Werema alisema mizaha katika Bunge hilo haina tija, hivyo
kususia kwa baadhi ya wajumbe hakuzuii kuendelea kwa majadala huo.
“Ninawaomba waliokubali kuendelea na mjadala huu tuwahi kesho,” alisema Jaji Werema.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan aliwataka wajumbe
hao kuwahi mapema saa 3:00 asubuhi ili kuendelea na kikao.
Kuhusu
ombi la mwongozo kutoka kwa mjumbe wa Bunge hilo, Mwigulu Nchemba
kuhusu kitendo na hatima ya wajumbe waliosusia kikao na kutoka
nje, Makamu Mwenyekiti huyo alisema itajulikana baaada ya Kamati ya
Uongozi wa Bunge Maalum la Katiba kukutana.
NA EDDY BLOG
0 comments:
Post a Comment