Mkurugenzi
wa shirika lisilo la kiserikali la Evidence for Action (E4A)
Tanzania,Craig John Felar, akitoa mada yake juu ya kampeni ya ‘Muokoe
Mama muokoe mtoto mchanga’ (Mama ye) kwenye semina iliyohudhuriwa na
baadhi ya viongozi kutoka vilabu vya waandishi habari mikoa mbalimbali
nchini .Semina hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na UTPC,ilifanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Lion hotel jijini Dar.
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vilabu vya waandishi wa habari Tanzania
,wakifuatlia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya uhabarisho juu
ya kampeni ya ‘Muokoe Mama na Mtoto Mchanga’ inayosimamiwa na shirika
lisilo la kiserikali la Evidence for Action (E4A) Tanzania
likishirikiana na Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania
(UTPC).
Bango linalohamasisha ushiriki wa kampeni ya ‘Muokoe Mama na Mtoto Mchanga’(mama ye).(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu,
SHIRIKA
Lisilo la kiserikali la Evidence for Action (E4A) Tanzania limesema
wanawake wajawazito 8,500 kufariki dunia wakati wa ujauzito au kwa
matatizo ya uzazi kila mwaka nchini.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa (E4A)
Tanzania, Craig John Felar wakati akiwahabarisha baadhi ya viongozi wa
vilabu vya waandishi wa habari nchini juu ya kampeni ya ‘Muokoe mama na
Mtoto Mchanga’
Aidha,amesema watoto wachanga 50,000,hufariki dunia ndani ya mwezi wa kwanza baada ya kuzaliwa.
“Kutokana
na takwimu hizo,kwa mwaka Tanzania,inapoteza wakazi wote wa vijiji 20
kama wakazi wake wanakuwa zaidi ya 1300″,amesema.
Amesema
waandishi wa habari nchini wanatakiwa kutumia kalamu zao kikamilifu
katika kuielimisha jamii juu ya afya ya mama na motto ili lengo la
kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga liweze
kufikiwa.
Amesema
tasnia ya habari nchini inaweza kutoa mchango mkubwa katika kupunguza
vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga endapo waandishi wa
habari watatambua kwamba wanalo jukumu kubwa na kuzuia vifo hivyo
kupitia kalamu zao.
Felar
alitaja baadhi ya hatua ambazo waandishi wa habari wanaweza kuzichukua
katika kusaidia kupunguza vifo hivyo ni kujenga ufahamu miongoni mwa
viongozi na jamii kuhusu hatua zinazoweza kuwaokoa watoto wachanga na
akina mama wajawazito.
Alitaja
hatua zingine kuwa ni kuwahimiza wanawake kujifungulia kwenye vituo vya
huduma za afya na si majumbani na kuhamasisha uwepo wa maandalizi ya
kumwezesha mama mjamzitio kujifungulia katika kituo cha huduma za afya,
Maandalizi hayo yawe ni kwa ajili ya gharama za usafiri,chakula na
usindikizaji.
Amesema
kutokana na hali hiyo, upo umuhimu mkubwa kwa waandishi wa habari
kushiriki kikamilifu na kuhakikisha kampeni ya ‘muokoe mama na mtoto
mchanga’,lengo la kupunguza vifo vya nakundi hayo,liweze kufikiwa mapema
iwezekanavyo.
Wakati
huo huo,Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania
(UTPC),Abubakar Karsan amesema kuwa umoja huo umeongeza vilabu vipya vya
mkoa wa Geita na Simiyu baada kutimiza ya kuwa wananchama.
Amesema
kuanzia sasa vilabu vyote vya waandishi wa habari mikoani ambao ni
wanachama wa UTPC,vitapatiwa hati maalum kuonyesha kuwa ni wanachama wa
UTPC.
CHANZO:MO-BLOG
0 comments:
Post a Comment