Wazazi wa takriban watoto
miamoja waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi
la Boko Haram wameingia msituni kuwatafuta watoto wao.
Wasichana hao walitekwa nyara kutoka shuleni mwao katika eneo moja la vijijini Kaskazini Mashariki mwa Nigeria Jumatatu usiku.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria
anasema kuwa ni hatari sana kwa wazazi hao hata kutafakari kuingia
msituni , kwani wapiganaji wa Boko Haram wamewaua mamia ya watu mwaka
huu , kwa kuwakata vichwa vyao.
0 comments:
Post a Comment