Idadi ya watu waliofariki jijini Dar es Salaam kutokana na mafuriko
yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika Ukanda wa Pwani
Mashariki imeongezeka kutoka wanane hadi kufikia 13.
Mkuu wa Mkoa huo, Saidi Meck Sadiki, alithibitisha kuongezeka kwa watu waliofariki dunia kutokana na mvua hizo zilizoanza kunyesha Ijumaa ya wiki iliyopita.Hata hivyo, alisema hana taarifa kamili ya idadi ya watu walioripotiwa kuathirika na mvua hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema miongoni mwa waliokufa ni pamoja na mtoto Lainat Ramadhan (2), baada ya kutumbukia kwenye shimo lililojaa maji jirani na nyumbani kwao, juzi saa 5:00 asubuhi katika eneo la Chanika Vikorongo, alipokuwa akimfuata mama yake nje.

CHANZO:NIPASHE
0 comments:
Post a Comment