Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa shule ya mabweni ya wasichana
imeshambuliwa katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
huku wasichana wakitekwa nyara.
Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili wametekwa nyara na washambuliaji hao.
Washambuliaji wanaaminika kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa
wanajeshi wawili waliuawa huku mali ikiharibiwa wakati wa shamblizi hilo
mjini Chibok.
Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi ya watu 70, waliuawa katika milipuko miwili ya mabomu katika kituo cha mabasi mjini Abuja.
Kundi la Boko Haram pia limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo.
CHANZO:BBC
0 comments:
Post a Comment