Awaomba
radhi wananchi wa Karema kwa kuchelewa kukamilika kwa mradi wa bandari
ambao umesimama kabisa baada ya mkandarasi aliyepewa mradi huo kushindwa
kuumaliza .
Asikitishwa
na watumishi wengi wa serikali kuendeleza tabia ya umangi meza kwani
miradi mingine inasimama kwa kipindi kirefu kwa sababu kuna kiongozi wa
serikali amechelewa kujibu barua itakayofanikisha mradi kuendelea na
kumalizika kwa wakati.
Asisitiza
Viongozi na wana CCM kuwa wakali katika kusimamia utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi na kusema si vyema tusubiri wapinzani waseme ,tunayaona
matatizo inabidi wana CCM wayasemee wenyewe na si vinginevyo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa
Kapalamsenga ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM inazidi kuimarika
na kuzidi kuaminika kwa wananchi siku hadi siku .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungmza mbele ya waandishi wa
habari kwenye eneo lililopaswa kujengwa bandari ya Karema baada ya
kujionea mradi wa ujenzi wa bandari ya Karema ulivyosimama.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia majengo yaliyokuwa
yameenza kujengwa kisha mradi wa ujenzi wa bandari kusimama kwa muda
mrefu,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya siku tatu mkoani Katavi ambapo
moja ya shughuli atakazofanya ni kukagua utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi na kujenga na kuimarisha Chama.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiongozana na Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye , Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk. Rajab
Rutengwe wakikagua mradi wa Ujenzi wa Mwalo uliopo kijiji cha Ikola.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mbunge wa Mpanda
Vijijini Ndugu Moshi Selemani Kakoso wakati wa kukagua mradi wa ujenzi
wa Mwalo katika Kijiji cha Ikola ambao utasaidia kuongeza thamani ya
samaki,mradi huu una thamani wa zaidi ya millioni 700.
CHANZO:MO-BLOG
0 comments:
Post a Comment