WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amewataka wahandisi wote nchini
kutokwenda likizo kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka hadi miundombinu
iliyoharibiwa na mvua itakapokamilika kukarabatiwa.
Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati wa
kuiaga na kuizindua Bodi mpya ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme
(Temesa).
Alisema kutokana na kuharibika kwa miundombinu mbalimbali nchini
hakuna haja ya mhandisi kwenda likizo hata akiwa katika hali ngumu.
“Watanzania wanategemea miundombinu ya barabara na madaraja katika
kupitisha mizigo na vyakula pamoja na shughuli za maendeleo, hivyo kazi
hii inapaswa kufanyika na kukamilika haraka,” alisema.
Alisema kunahitajika nguvu za ziada katika kutekeleza hilo, ndiyo
maana ameamua kukatisha likizo za wahandisi ili kufanikisha hilo.
“Nafanya ziara za ukaguzi katika maeneo yote yaliyoathrika na
nikibaini kuna mhandisi kaenda likizo basi afungashe virago vyake huko
huko na asirudi tena,” alisema.
Alitaja baadhi ya madaraja yaliyoanza kukamiliki na kutumika kuwa ni
Daraja la Lindi linaloungana na Kongowe, Daraja la Mpiji Magohe na
Bagamoyo ambalo hadi sasa limekamika katika tuta kiasi cha mita 75
pamoja na Daraja la Ruvu ambalo linatumika upande mmoja.
Mbali na hayo, aliitaka Bodi mpya ya Temesa kuwa makini katika
shughuli zake, kwani ni miongoni mwa wahusika wakubwa pia wanaowajibika
katika utekelezaji wa miundombinu nchini.
CHANZO:EDDY BLOG
0 comments:
Post a Comment