Viongozi wa operesheni ya kuitafuta ndege ya Malaysia
ya MH370 iliyotoweka mwezi mmoja uliopita, Angus Houston wa Australia,
amesema kuwa ametambua mawimbi ya sauti inayoaminika kutoka kwa kinasa
sauti cha ndege hiyo maarufu kama 'black box' ya ndege hiyo.
Houston alisema kuwa kifaa maalumu
kinachokokotwa na meli moja ya kijeshi ya Australia, Ocean Shield,
kilipata mawimbi kamili kwa muda wa kati ya dakika tano u nusu na saba.
Mawimbi sawa na hayo yaliopatikana mwishoni mwa
wiki na hii ina maana kuwa wataweza kulenga eneo ambalo inaaminika zaidi
kuwa ndege hiyo ilianguka na kwa hivyo kuimarisha utafutaji wake.
0 comments:
Post a Comment