Zaidi ya shilingi
million 30 za mfuko wa jimbo zimetolewa wilayani makete katika kutekeleza
miradi mbalimbali katika sekta ya elimu,maji afya, nishati na barabara.
Akitoa taarifa ya ugawaji
wa fedha hizo mwenyekiti wa kamati ya ugawaji wa fedha hizo na mbunge wa jimbo
la Makete Dr. Binilith mahenge amesema pesa hizo hutolewa kama chachu ya
maendeleo na sio kumaliza matatizo kabisa katika jamii na kuwaomba wananchi kurithika
na kidogo kilichotolewa.
Nae katibu kamati hiyo
ndugu Cyras kapinga ameyataja maeneo yaliyo pata fedha hizo kuwa ni kata zote wilayani makete katika
sekta za elimu, maji, afya ,nishati na barabara, na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo diwani viti maalum Tarafa
ya Magoma Mh Sarah Shembekeza ameushukuru mfuko huo kwa kuwa chachu ya
maendeleo wilayani na kuongeza kuwa watendaji katika maeneo tofauti wasimamie
kikamilifu fedha hizo
0 comments:
Post a Comment