Home » » WATU ZAIDI YA 12 WAFARIKI PAPO HAPO BAADA YA BASI KUGONGA NYUMBA NA KUPINDUKA MKOANI SIMIYU

WATU ZAIDI YA 12 WAFARIKI PAPO HAPO BAADA YA BASI KUGONGA NYUMBA NA KUPINDUKA MKOANI SIMIYU

Written By kitulofm on Monday, 21 April 2014 | Monday, April 21, 2014

Picha na Eddy Blog
Watu zaidi ya 20 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya wilayani Busega Mkoani Simiyu leo asubuhi kufuatia ajali ya Bus la kampuni ya Luhuye iliyopasuka mpira, kuacha njia na kugonga nyumba.

Mbunge wa Jimbo la Busega ambaye pia ni Waziri wa uvuvi na maendeleo ya Mifugo Dakta Titus Kamani ameiambia Blog hii kwa njia ya Simu kwamba ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sogesita wilayani humo.

Dakta Kamani amesema basi hilo lilikuwa likielekea Jijini Mwanza ndipo lilipopasua mpira wa mbele na kupinduka huku likigeukia lilikotoka kabla ya kuacha njia na kugonga nyumba kwenye kaya moja kijijini hapo.

Amesema, idadi kamili ya waliopoteza maisha na hali za majeruhi itafahamika baadaye 
Chanzo:farajimfinanga.com
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm