Rais
Jakaya Kikwete akizungumza kwenye uzinduzi wa kongamano la 19 la mwaka
la utafiti liliandaliwa na taasisi ya utafiti nchini REPOA. Rais Kikwete
alilisitiza kwamba utafiti nchini kwa wafanyabiashara ndogo ndogo na
vijana kwa ajili ya kupambana na umaskini ni umuhimu kwa maslahi ya
vizazi vya sasa na vijavyo. Utafiti huo wa REPOA ulijikita katika
mabadiliko ya uchumi na kilimo na kujenga mazingira mazuri kwa
wafanyabiashara ndogo ndogo na za kati na kupanua wigo wa ajira kwa
vijana na wakinamama.(Picha na Freddy Maro).
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa
REPOA, Profesa Samwel Wangwe baada ya kuzindua kongamano la 19 la mwaka
la utafiti liliandaliwa na taasisi ya utafiti nchini REPOA.(Picha na
MOblog).
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
RAIS
Jakaya Kikwete amewahakikisha watanzani serikali ipo katika hatua za
mwisho kuandaaa sheria, kanuni na utaratibu kwenye sekta ya gesi na
mafuta kwa ajili ya uwekezaji wenye tija nchini.
Akizungumza
kwenye kongamano la 19 la mwaka kwenye uzinduzi wa ripoti ya ya utafiti
wa Shirika Lisilo kuwa la Kiserikali la (REPOA) linalofanyika jijini
Dar es Salaam kwa siku mbili, Rais kikwete alisema mpaka mwezi oktoba
mwaka huu serikali itakuwa imeweka sheria, kanuni kwenye sekta ya gesi
na mafuta ili wazawa washiriki kikamilifu.
“mpaka
ukifika mwezi Oktoba basi sheria na taratibu zote zitakuwa tayari na
kufungua milango pia kwa wawekezaji wa ndani kushiriki kwenye sekta ya
gesi na mafuta nchini,” amesema
Amesema
kwamba kwenye uwekezaji wa gesi na mafuta taifa litapata manufaa
makubwa na mabilioni ya pesa yataingia kwa hiyo ni nafasi muhimu pia kwa
watanzania wenye biashara za kati na ndogo ndogo kunufaika na uwekezaji
huo.
Rais
Kikwete alisisitiza kwamba katika uwekaji wa sheria na taratibu lazima
mambo ya urasimu na rushwa viondolewe mara moja ili kuhakikisha sekta
hiyo inakuwa na manufaa kwa wananchi wote.
Aliongeza
kwamba lazima serikali na wadau wote muhimu wajiridhishe kwamba hakuna
wizi wala utapeli katika sekta gesi na mafuta ili kumletea mwananchi wa
kawaida maendeleo.
Kikwete
alifafanua kwamba lazima serikali ihakikishe inajipanga vizuri ili
kuzuia vitendo vyovyote vya hujuma, wizi na rushwa ili kuleta matokeo
chanya kwa nchi na watu wake.
Amesema
kwamba kwa muda mrefu watafiti wa ndani wamekuwa na msaada mkubwa
katika kuisaidia serikali kutambua maeneo yenye mahitaji zaidi na hasa
katika kuboresha maisha ya wananchi na kupambana na tatizo la ajira
nchini.
“tafiti
hizi za kila mwaka zimekuwa na msaada mkubwa kwa wafanyabiashara wadogo
wadogo, wakulima na wananchi wa kawaida katika kufanya uamuzi sahihi
kwenye maeneo,” aliongeza
Amesema
kwamba nchini Tanzania zipo ajira ndogo ndogo milioni tatu lakini
wanaofanya ajira hizo ni milioni tano na laki mbili kati hao asilimia 64
ni wanawake.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Profesa Samwel Wangwe
amesema kwamba tafiti hizi zinalenga kuwasaidia wananchi
wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kupunguza umaskini.
Profesa
Wangwe amesema kwamba malengo ya tafiti pia ni kuongeza tija kwa kupata
uzoefu kutoka nchi mbalimabali ulimwenguni ya jinsi ya kujenga viwanda,
kusindikaji wa chakula na kupambana na tatizo la ajira hasa kwa vijana
na wanawake.
Aliongeza
pia kwamba REPOA wamewaalika wataalamu mbalimbali kutoka nchini ya
Japan ili watanzania waweze kujifunza kutokana na nchi zao katika
harakati za kupambana umaskini Afrika.
0 comments:
Post a Comment