Shule ya msingi Ndulamo
iliyopo katika Kijiji cha Ndulamo Kata ya Iwawa wilayani Makete Mkoani Njombe
inakabiliwa na tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa
Darasa moja hutumiwa na
zaidi ya wanafunzi 94-100 jambo ambalo husababisha msongamano kwa Wanafunzi katika
darasa moja ambapo serikali imeombwa msaada wa kuongeza majengo ili kuendana na
idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hapo
Hayo yamesemwa na Mwl.
Mkuu wa shule ya Msingi Ndulamo Bw.Godigodi Malangalila alipokuwa akizungumza
na kitulo fm na kubainisha kuwa vyumba vya madarasa vilivyopo haviendani na
idadi ya wanafunzi shuleni hapo na kusema kuwa wakati mwingine hulazimika
kuwaambia wanafunzi watoe masweta kutokana na hali nzito ya hewa pindi wawapo
Darasani
Mbali na tatizo hilo
amesema bado kuna tatizo la uhaba wa walimu ambapo hadi sasa shule hiyo ina
jumla ya walimu 14 tu na kuongeza kuwa masomo ambayo yana upungufu sana wa
walimu ni somo la hisabati,kiingereza pamoja na sayansi katika
Pia Mwl.Godogodi ameongeza
kuwa shule ya msingi Ndulamo ina tatizo kubwa la watoto yatima mpaka sasa shule
hiyo ina jumla ya watoto yatima 111 na kupongeza juhudi zinazoendelea kufanywa
na wananchi wa kijiji cha Ndulamo ambao wana mfuko maalumu kwa ajili ya
kuwasaidia watoto yatima katika kijiji hicho na kuomba watu wenye moyo wa kusaidia
wawasidie watoto hao kwa msaada wowote hasa mahitaji ya shuleni ili kuwasaidia
watoto hao kuendelea na masomo.
0 comments:
Post a Comment