CHANZO:BBCSWAHILI
Idhaa ya BBC kitengo cha Afrika kimebaini ushahidi wa watu wanaonunua
matokeo bandia ya vipimo vya virusi vya HIV yakionyesha hawana virusi
hivyo nchini Uganda.
Picha za Filamu zilizochukuliwa kisiri zinaonyesha namna ilivyo rahisi
kutoa hongo kwa wahudumu wa afya ili kupata vyeti hivyo bandia.
Baadhi ya watu wanaonunua vyeti hivyo visivyokubalika kisheria
wanasema wamefanya hivyo ili kupata kazi, kusafiri kwenda ng'ambo ama
kwa ajili ya kupata wapenzi wa ngono.
Mwandishi wa BBC wa Kampala Catherine Byaruhanga alilitembelea kliniki 15 bila kujitambulisha.
Kumi na mbili kati ya kiliniki hizo zilikuwa
tayari kutupa vyeti bandia vya kuthibitisha kuwa hatuna virusi vya
kusababisha ukimwi vya HIV.
Wanaosimamia kliniki hizo walitaka hongo kati ya Dola 10 na 20 kwa kila cheti.
Picha za video tulizopiga kisiri katika maduka
ya kupiga chapa katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Uganda Kampala
zinathibitisha kuwa unaweza kuigiza cheti pia kwa urahisi sana.
Tulipomkabidhi Waziri wa Afya, Ruhakana Rugunda,
ushahidi wetu, alikubali kuwa hiyo ni changamoto kubwa lakini
akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila juhudi kuwakamata na kuwashtaki
wanaohusika
katika ufisadi huo.
Serikali ya Marekani hutoa kiwango kikubwa cha peza za miradi inayotumiwa kupambana na ukimwi nchini Uganda.
Balozi wa Marekani alitoa wito kwa viongozi wa taifa hilo kufanya bidii zaidi kupambana na kashfa hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa hana uhakika kuwa Dola za Marekani hazijatumiwa katika kliniki hizo zinazotoa vyeti bandia.
0 comments:
Post a Comment