Wananchi
wa Makete mjini, wilayani Makete mkoani Njombe, wameombwa kuwa na
subira kufuatia kukosekana kwa huduma ya maji tangu jana na kusababisha
usumbufu kwao huku wengine wakichota maji mtoni kwa ajili ya matumizi
yao
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja wa mamlaka ya maji Makete mjini Bw. Yonas
Ndomba (Pichani) wakati akizungumza na mwandishi wetu Veronica Mtauka,
na kusema tatizo hilo la ukosefu wa maji limetokana na kupasuka kwa
bomba la maji katika kijiji cha Ivalalila na kusababisha maji kuishia
hapo na kutofika Makete mjini
Bw.
Ndomba amesema kwa sasa mafundi wake wamefika eneo la tukio tangu jana
na kuendelea kulitengeneza bomba hilo ambapo kwa jana walishindwa
kulikamilisha lakini kwa hivi sasa wapo eneo la tukio wanaendelea na
matengenezo na wanaimani kazi hiyo itamalizika leo na huduma ya maji
itarejea kama kawaida kwa wateja wake
Amesema
tatizo hilo limesababishwa na ubadilishaji wa mabomba ambapo anadhani
wakati wakubadilisha mambomba hayo huwenda yabondwa kwa bahati mbaya na
kuweka nyufa na ndiyo maana limepasuka kwa kuwa kwa sasa idara yake
inaendelea kufanya marekebisho mbalimbali ili kuongeza wingi wa maji
Makete mjini
"Kwa
sasa kuna mabomba tunayafukua sehemu moja na kuja kuyahamishia sehemu
nyingine, hivyo wakati wa ufukuaji inawezekana bomba likagongwa na
kupata hitilafu na wakati wa kulifunga halionyeshi tatizo ila baada ya
kupita siku kadhaa ndiyo unakuta yanapasuka kama hivi" amesema Ndomba
Hata hivyo kufikia jioni ya leo
tatizo hilo limetatuliwa tayari na maji yameanza kupatikana katika maeneo yote
ambayo yalikuwa hayapatikani tokea jana
Na Veronica Mtauka
0 comments:
Post a Comment