Home »
» HII SASA NI KUFURU!!! P-SQUARE WAWEKA SOFA{SAMANI} ZA DHAHABU NDANI YA NYUMBA YAO MPYA
Hakuna ubishi kuwa, kwa hiki walichokifanya sasa, na kama macho yetu
hayatudanganyi kwa hiki yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama
hii inayoonekana ni dhahabu kweli, basi P-Square, hela wanayo.
Peter ameshare picha hizi nne ambazo wiki hii zitakuwa gumzo barani
Afrika ambapo kwenye picha moja inayomuonesha pacha mwezie Paul akiwa
amesimama kwenye sebule mpya inayoaminika kuwa ya nyumba yao mpya,
ameandika ‘Goldenworld #blessed.’
Kwenye picha nyingine, wanaoonekana wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo
iliyotawaliwa na kile kinachoonekana kama dhahabu zilizozunguka sofa za
kuvutia na Peter ameandika: #2kings…… Work hard,play harder.’
Picha nyingine inamuonesha Peter akiwa peke yake kwenye meza ya chakula,
kubwa, iliyojaa vyombo vya thamani vya kuvutia na ameandika: A king in
my own world…. #Blessed.”
Hawa jamaa ni noma
0 comments:
Post a Comment