Home » » WANAHABARI WILAYANI MAKETE WAASWA KUTUMIA TAALUMA YAO IPASAVYO

WANAHABARI WILAYANI MAKETE WAASWA KUTUMIA TAALUMA YAO IPASAVYO

Written By kitulofm on Wednesday, 18 December 2013 | Wednesday, December 18, 2013

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiFWuP9o9bzSAbEpn_Dqr99WqHWUVIXzmpPgoMctF88LwR2BAdh85ro0ANTnEdosj8aDmRISsZvlW4kxi5MWgKnHIKiyV3PNXySFwk94fy4zMAvYI1YM3Wa66bBLIOpG4cE8LaRLqhyphenhyphenSRE/s1600/DSC00150.JPG

Waandishi wa habari wameaswa kufuata maadili ya taaluma yao ili kutoviingiza vyombo vya habari katika matatizo na kuipotosha jamii

Wito huo umetolewa siku ya jumatatu na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh.Daniel Okoka aliyekuwa mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo ya kuijengea uwezo bodi ya redio Kitulo fm pamoja na wakuu wa Idara kwa ufadhili wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini Tanzania Media Fund(TMF) mafunzo hayo yatakayochukua siku 5 kuanzia jana hadi Ijumaa ya tarehe 21 Desemba mwaka huu

Katika mafunzo hayo yalihodhuriwa na wanahabari kutoka Kitulo fm redio,bodi ya redio na muwezeshaji Dr.Alfred Rwechengula katika kuhakikisha redio inaingiza kiasi kikubwa cha  mapato kwa njia ya uboreshaji wa vipindi vyenye kuelimisha jamii

Jumla ya wanahabari 10 wameanza kupata mafunzo hayo ili kuelimisha jamii ya wanamakete na nje ya Makete pia ili kuongeza uelewa kwa wanajamii hasa katika Nyanja ya Elimu ,Afya, Mazingira pamoja na Biashara

Mh.Okoka ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na wananchi kupata habari za Makete na duniani kwa ujumla kwa wakati muafaka,kuwahamasisha vijana kujishughulisha na maendeleo ktk jamii,imetoa ajira kwa vijana wenye taaluma ya uandishi wa habari na Utangazaji,imesaidia kutangaza matangazo ya halmashauri na kuwafikia walengwa kwa wakati

Hata hivyo amezitaja baadhi ya changamoto ambazo redio inakumbana nazo kuwa ni pamoja na vifaa duni hivyo kutofikia baadhi ya maeneo hata katika wilaya ya makete,kituo kinaingiza mapato kidogo pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wanahabari waliopo kituoni hapa
 
Redio kitulo fm ambayo ilianzishwa mwaka 2005 kwa msaada wa UNICEF kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Makete


Na Furahisha Nundu
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm