Habari zilizotufikia usiku huu ni kwamba kumetokea ajali mbaya za pikipiki maarufu kama bodaboda kugongana wilayani Makete mkoani Njombe
Ajali hiyo imetokea usiku huu majira ya saa 4:22 eneo la Kona Makete ambayo imehusisha pikipiki mbili aina ya SANLG zenye namba za usajili T 280 BJR na nyingine ni T 878 BKU
Madereva wote wawili ambao majina yao hayakufahamika mara moja wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Makete kwa matibabu zaidi
Habari zaidi zitakujia muda wowote kuanzia sasa kutoka kwa mwandishi wetu Furahisha Nundu ambaye yupo eneo la tukio
0 comments:
Post a Comment