Home » » WAZAZI MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUWAENDELEZA WATOTO WAO KITAALUMA

WAZAZI MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUWAENDELEZA WATOTO WAO KITAALUMA

Written By kitulofm on Tuesday, 17 December 2013 | Tuesday, December 17, 2013



Wazazi Mkoani Njombe Wametakiwa Kuwaendeleza Watoto Wao Kitaaluma Ikiwa ni Pamoja na Kuwapatia Mafunzo ya Fani  Mbalimbali  Zinazotolewa na Taasisi za vyuo Vilivyopo Mkoani Njombe, Jambo Ambalo litasaidia Kupunguza Tatizo la Ajira Miongoni Mwa Vijana Mkoani Njombe.

Akizungumza Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Benki ya NJOCOBA  Wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Cha Utalii na Uandishi wa Habari Cha  Eckros Njombe,Mwakilishi wa Mkurugenzi Bw Mfikwa Amesema Kuwa Vijana Wanaweza Kuondokana na Tatizo la Ajira Endapo Wataendelezwa Kitaaluma na Hivyo Kuwataka Wazazi Kutokata Tamaa Dhidi ya Vijana Hao.

Amesema Pamoja na Mambo Mengine Uongozi wa Chuo Unatakiwa Kutatua Baadhi ya Changamoto Zinazokikabili Chuo Hicho Ili Kuhakikisha Inaboresha Hali ya Taaluma na Kiwango Cha Elimu Inayotolewa Chuoni Hapo Jambo Litakalosaidia Kuwa na Wahitimu Wenye Uwezo Kitaaluma na Kufanya Kazi Kwa Ubora.

SOMA ZAIDI;eddy blog
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm