Habari na Elia Kimani,Picha na Furahisha Nundu
Wananchi wa kijiji cha
Matenga ktk kata ya Ikuwo wilayani Makete mkoani Njombe wameiomba serikali
kuwatengenezea barabara ya kutoka ujuni kwenda Ikuwo kwani kuna tatizo kubwa
hasa kwa kipindi cha Masika.
Akizungumza kwa niaba ya wananchin
wa kata hiyo Diwani wa kata hiyo Mh.Antony Sanga amesema miundombinu ya
barabara ktk eneo hilo imekuwa changamoto kwani inapitika kwa shida hasa
kipindi hiki cha masika.
Pia amesema kuwa wakazi na
wasafiri walio wengi hulazimika kutumia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ambapo kutoka Ikuwo kwenda Maakete mjini ni
sh.elfu 30 kitu ambacho kwa wanachi wa Makete ni vigumu.
Pamoja na hilo amesema kuna changamoto ya kutokuwepo
kwa huduma ya mawasiliano tokea kuanza kwa huduma za simu wananchi wamekuwa
wakipata mawasiliano kwa kusimama juu ya miti na milimani.
Hata hivyo ametumia fursa
hiyo kuwashukuru wananchi wa kata ya Ikuwo kwa jitihada za kuendelea na ujenzi
wa wodi kwani kwa sasa wapo ktk hatua za mwisho za ukarabati wa jengo hilo .
0 comments:
Post a Comment