Na Furahisha Nundu
Wafanyabiashara wenye
vibanda katika kitongoji cha Dobwela
Kijiji cha Iwawa Kata ya Iwawa
Wilayani Makete wamewataka
wafanya biashara kuwa na ulinzi ili kulinda mali zao.
Wameyasema hayo katika
mkutano uliyofanywa na umoja wa watu wenye vibanda Dobwela uliofanywa ili kujadiri jinsi ya kulinda mali zao
za biashara katika kitongoji hicho.
Mkutano huo uliyo kuwa chini
ya makamu mwenyekiti wa kitongoji hiho Bw.Henry
Mahenge ambapo umoja wa wanakikundi hao wamesema ni vema kuwepo ulinzi katika eneo hilo ili kufanya biashara zao kwa amani na umoja bila kuwa na shaka yoyote.
"Ili tufanye biashara zetu kwa amani ni lazime tuhakikishe tumeweka ulinzi katika eneo hili la Dombwela mbona wenzetu maeneo mengine kama Mabehewani,Sokoni wameweka walinzi?"Alizungumza mmoja kati ya wanye vibanda eneo hilo
Hivyo wameadhimia kuajiri
ulinzi ili wawasaidie kulinda kwani watakuwa wanachangia kila mwezi ili kuwalipa walinzi hao mali zao ziendelee kuwa katika hali
ya usalama.
0 comments:
Post a Comment